FAIDA 10 ZA TANGAWIZI MWILINI
Huwa nafurahi sana ninapoutafakari ukubwa wa M/Mungu kwa namna ambavyo ametupa mimea mbalimbali muhimu kwa ajili ya afya zetu. Maelezo yafuatayo kuhusu tangawizi yatakupa wewe ujuzi wa mmea mwingine wa asili usio na madhara ya kikemikali na kusaidia mwili wako kuwa na afya nzuri na ya kupendeza.
Tafiti mpya zinazidi kuonyesha namna mmea huu ulivyo wa mhimu kwa afya ya binadamu ikihusisha uwezo wake wa kushughulika na aina mbalimbali za saratani mwilini na tafiti nyingine zinaendelea kufanyika.
Tangawizi inaweza kuwekwa karibu kwenye kila chakula, iwe ni katika kuilainisha nyama nyekundu, kuongeza ladha katika nyama au samaki, kama chai, kwenye juisi na kadharika. Binafsi napenda ikiwa kwenye juisi ya matunda ndiyo inakuwa tamu zaidi na inaenda kufanya kazi mwilini haraka zaidi.
Tangawizi iliorodheshwa kwa mara ya kwanza na serikali ya Marekani kama dawa kwa ajili ya binadamu kati ya mwaka 1820 na 1873.
Tangawizi huongezwa pia katika vinywaji vingi vya viwandani zikiwemo soda ili kupata radha nzuri zaidi.
FAIDA ZAKE
1️⃣Huondoa harufu mbaya ya kinywa,
Tofauti na vyakula vingine kama kitunguu swaumu, tangawizi husaidia uwe na harufu nzuri pale unapopumua na kufanya maeneo ya kinywa chako kuwa safi
2️⃣Tangawizi husaidia msukumo wa damu kuwa mzuri,
Tangawizi husaidia msukumo wa damu mwili kuwa vizuri hii ni kwa sababu huupa mwili joto la kutosha pindi unapokunywa chai ya tangawizi ambapo mwili huhitaji wakati wa usukumaji wa damu mwilini
3️⃣Huondoa magonjwa ya asubuhi,
Tanagawizi licha ya kuwa ni tiba ya magonjwa kama kikohozi na mafuta mwilini, tangawizi pia husaidia kupunguza magonjwa ya asubuhi kama uchovu na mninginio, kwa akina mama hasa wajawazito tangawizi huwapunguzia homa za asubuhi pindi wanapoamka , pia hutumika kama kichocheo cha utulivu.
4️⃣Tangawizi husaidia mfumo wa chakula mwilini
Tangawizi husaidia mwili kunyonya virutubisho kwenye chakula hii husaidiana sana pale unapoamua kupunguza uzito wa mwili na kupata virutubisho vilivyo muhimu tu.
5️⃣Tangawizi hurekebisha sukari ya mwlii
Husaidia katika kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu, hapa wagonjwa wa kisukari wanashauriwa kutumia tangawizi badala ya chai,
6️⃣Tangawizi huongeza hamu ya kula
Huongeza hamu ya kula chakula kwa wale wenye mfumo mbaya wa umeng’enyaji wa chakula wanashauriwa kutumia tangawizi ili kupata mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula
7️⃣Tangawizi husaidia kuyeyusha mafuta mwilini
Tangawizi husaidia kupunguza kuganda kwa mafuta mwilini ambayo yana madhara makubwa mwilini hasa magonjwa ya kiharusi na shinikizo la damu.
8️⃣Tangawizi husaidia kuondoa sumu mwilini
9️⃣Tangawizi husaidia kuondoa kichefuchefu na kutapika pia huwasaidi sana wale watu waliotumia sana madawa na kuwa sumu nyingi mwilini
🔟Tangawuzi husaidia kutibu vidonda vya tumbo
Tangawizi pia husaidia mtu mwenye vidonda vya tumbo kwa kupunguza maumivu na hata kuponya vidonda hivyo kama vitakuwa katika hatua ya awali.
*FAIDA NYINGINE:*
Tanagawizi ina kiinilishe muhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za saratani ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu (gingerol) vilevile hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu kwa kitaalamu (constipation related cancer).
Huzuia kuzalishwa kwa bacteria aitwaye (helicobacter pylori) bacteria huyu ndiye anayesababisha vidonda vya tumbo mwilini pia hutibu kiungulia na kazi mbali mbali za tumbo.
Pia husaidia katika kutibu kansa ya titi,
Pia tangawizi husaidia kutibu kansa za kwenye kizazi na kansa za kwenye mirija ya uzazi.
Husaidia kuzuia shambulio la moyo,
⇰Huzuia damu kuganda,
➡️Hushusha kiwango cha kolesto,
➡️Husafisha damu
➡️Husaidia watu wenye kukamaa mishipa
➡️Hutibu maumivu ya tumbo hasa wakati wa hedhi,
➡️Huimarisha afya ya figo
✍🏻Ina madini ya manganese ambayo ni muhimu kuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali,
➡️Hulinda kuta za moyo,
➡️Hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita.
Tangawizi inakitu kiitwacho (silicon) ambacho cheyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha pia husaidia umengenyaji wa madini ya calcium.
Tangawizi ina vitamin A, C, E, B complex, chuma, zinki, magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta carotene (nzuri kwa Uzazi wa mwanaume na mwanamke).
Unaweza kujitibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia zao hili la tangawizi kwa kufuata maelekezo yafuatayo
Kwa wale wenye kuumwa jino na maumivu ya kichwa, unashauriwa kuchukua tangawizi ya unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope kisha jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala, kwa jino jipake na uchue kwenye shavu.
Kwa wenye maumivu makali ya tumbo unashauriwa kuwa changanya kijiko kimoja au viwili vya tangawizi iliyosangwa na kijiko kimoja au viwili vya asali kisha kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.
Kujitibu tatizo la kuvimbiwa nakukosa hamu ya kula, unashauriwa kuchangaya juice ya tangawizi, juice ya limao na chumvi mawe kwa vipimo vilivyo sawa hakikisha umechanganya vizuri kunywa dawa hiyo kabla ya kula chakula au changanya vipimo vilivyo sawa sawa vya juice ya tangawizi na sukari, koroga vizuri kunywa kabala ya kula chakula.
Dawa hii husafisha ulimi na koo na hukuongezea hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.
Kujitibu maumivu ya kukohoa na kukauka sauti unashauriwa kutafuna vipande vidogo vya tangawizi vilevile kujitibu tatizo la kuharisha unashauriwa kuchua sehemu zinazozunguka kitovu kwa juice ya tangawizi.
Tumia kwenye juice, mboga, tafuna, kwenye asali, chai au maji ya moto.