Nguvu za kiume ni nini?

Nguvu za kiume ni jina la jumla lenye vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na hamu ya mapenzi; kusimama kwa uume barabara; kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo la lenyewe.



Ni viungo gani vinavyohusika na nguvu za kiume? Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu 50 ndani ya mwili wa mwanaume vinavyohusika na nguvu za kiume ambapo viungo hivi pia hufanya kazi zingine za mwili. Baadhi ya viungo hivyo ni ubongo, moyo, mishipa ya neva mishipa ya ateri, mirija iliyo ndani ya uume iitwayo corpora cavernosa.

Viungo vingine ni neva maalumu za parasympathetic, tezidume (prostate gland), ini, figo, homoni ya testestorone, kemikali za acetylcholine, serotonin, na dopamine, uti wa mgongo, eneo la chini ya mgongo (kiuno), eneo la nyonga.

Viungo vingine ni misuli maalumu iitwayo pelvic floor, tezi pituitari (pituitary gland), utando maalumu wa uumeni uitwao tunica albuginea, misuli iitwayo pubococcygeus [PC muscles], kemikali ya nitric oxide, kemikali ya prolactin n.k. Hivi ni baadhi ya viungo vinavohusika katika kumaanisha Nguvu za kiume.

Nini maana ya kupungua nguvu za kiume? Unapopungua nguvu za kiume ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu katika vitu nilivyovitaja hapo juu havifanyi kazi vizuri jinsi ipasavyo na inavyotakiwa. Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homoni fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance), orodha ni ndefu sana.

Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo hutokea upungufu katika nguvu za kiume. Upungufu huo unaweza kuwa ni:👇👇👇

1. Kukosa hamu ya mapenzi,

2. Uume kusimama kwa uregevu,

3. Kuwahi kufika kileleni,

4. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa)

5. Kushindwa kurudia tendo la ndoa,

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo,

7. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji,

8. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu

Nguvu za kiume ni Topic ndefu sana lakini hata ivyo ni rahisi sana kuishi ukiwa mkamilifu katika tendo la ndoa kama mwanaume. Kama unakutana na dalili yoyote kati ya hizo apo juu basi una changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume, Jitahidi kufanya mazoezi walau mara tato kwa wiki, Kunywa maji kwa wingi, Kula saana Matunda na mbogo mboga, Punguza matumizi ya vilevi, Punguza msongo wa mawazo, Acha kupiga Punyeto, n.k

#nguvuzakiume #tendolandoa,